MBEYA YAKARIBIA KULAMBA LAMBALAMBA YA AZAM
Klabu ya Mbeya City, ipo anakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji Didier Kavumbagu, aliyekuwa ikiichezea Azam FC msimu uliokwisha hivi karibuni
Taarifa za ndani ya Mbeya City zinasema kwa asilimia kubwa, Kavumbagu raia wa Burundi na Mbeya City wamemalizana.
Katibu mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe ameiambia Goal, wapo katika hatua za mwishoni kukamilisha makaubaliano hayo ambayo waliyaanza siku chache zilizopita baada ya ligi kumalizika.
“Mazungumzo yetu yamefikia sehemu nzuri ingawa bado hatujaingia naye kwenye mkataba lakini siku chache zijazo mambo yanakwenda vizuri na huenda Kavumbagu akawa mchezaji wetu siku chache zijazo kama tutatimiza masharti anayohitaji,”amesema Kimbe.
Kavumbagu aliyewahi kutamba na Yanga, anataka kuchana na Azam kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza msimu uliopita jambo lililomfanya mara kwa mara kulumbana na kocha wake Stewart Hall.
Post a Comment