KIOO CHA AKISI

Tuna akisi mwangaza wa jua kwenye hii dunia bila kubagua rangi, kabila wala taifa.

KIASI CHA PROTINI KATIKA MWILI WA BINADAMU

    Protini ni molekuli ndefu na sehemu za lazima katika muundo wa seli za mwili waviumbehai. Zinajengwa na amino asidi. Protini huwajibika kwa maumbile ya seli na kushughulika usafirishaji wa dutu ndani ya seli na kati ya seli za mwili. Musulizinaundwa pamoja na protini za pekee zenye uwezo wa kupanua na kujikaza hivyo kuweka msingi wa mwendo.
Protini zinapatikana katika wanyamamimeafungi na bakteria.

Tumboni mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao; kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.
Uhaba wa protini unasababisha magonjwa; uhaba mkali unaleta unyafuzi. Unyafuzi unashika hasa watoto wanaopewa chakula kingi lakini kabohidrati tu kama ugali bila makundekundenyama au samaki.
vyakula vifwatavyo vina protini nyingi:
nyama
samaki
mayai
maziwa na vyakula kutokana na maziwa kama jibini, maziwa ya mgando
jozi
makundekunde kama soya, kunde, maharage.
      
TAMBUA
Kula nyama nyingi au samaki wengi sio kigezo cha kuwa utakua umeupa mwili mahitaji yake bali umeuongezea mzigo.Mwili huitaji kiasi kutokana na mahitaji yake.

    Namna ya kujua kiasi cha protini kinacho hitajika mwilini

         PIMA UZITO WAKO KISHA ZIDISHA KWA 0.8g 


       Muda mwingine tutakuja kuona umuhimu wa nyama na mboga, pia kipi  kinatoa msaada katika mwili kuliko kingine.

No comments

Powered by Blogger.