KIOO CHA AKISI

Tuna akisi mwangaza wa jua kwenye hii dunia bila kubagua rangi, kabila wala taifa.

CHINA YATANGAZA MARUFUKU KUFUNGA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI KWA WAISLAMU

Utawala wa China wa chama cha kikomunisti umetangaza kuweka marufuku ya kufunga mwezi wa Ramadhankwa Waislamu wa asili ya Uygur wanaoishi nchini humo.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa mtandanoni, utawala ulitangaza marufuku hayo kwa maafisa wa taasisi za serikali, wanafunzi na watoto wa Kiislamu wanaoishi katika eneo la Uygur.
Baadhi ya migahawa ya vyakula pia imeamuriwa kuachwa wazi na kuendeleza huduma zao za vyakula katika eneo la Uygur lililokuwa na Waislamu zaidi ya milioni 10.
Vile vile, maduka ya kuuza vyakula na vinywaji pia yameagizwa kuendeleza shughuli za biashara kama kawaida katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya viongozi wa miji kadhaa pia wametoa maelezo na kuarifu kwamba Waislamu hao hawapaswi kuingia misikitini.
Msemaji wa jamii ya Waislamu wa Uygur Dilshat Rashid alikemea hatua hiyo na kusema kwamba utawala wa China hauna haki ya kuingilia kati imani za wananchi.


SOMA HAPA
Waislamu wa China wapigwa marufuku kufunga Ramadhan

No comments

Powered by Blogger.