Tumboni mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao; kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.
Uhaba wa protini unasababisha magonjwa; uhaba mkali unaleta unyafuzi. Unyafuzi unashika hasa watoto wanaopewa chakula kingi lakini kabohidrati tu kama ugali bila makundekunde, nyama au samaki.
vyakula vifwatavyo vina protini nyingi:
nyama
samaki
mayai
maziwa na vyakula kutokana na maziwa kama jibini, maziwa ya mgando
jozi
makundekunde kama soya, kunde, maharage.
TAMBUA
Kula nyama nyingi au samaki wengi sio kigezo cha kuwa utakua umeupa mwili mahitaji yake bali umeuongezea mzigo.Mwili huitaji kiasi kutokana na mahitaji yake.
Namna ya kujua kiasi cha protini kinacho hitajika mwilini
PIMA UZITO WAKO KISHA ZIDISHA KWA 0.8g
Muda mwingine tutakuja kuona umuhimu wa nyama na mboga, pia kipi kinatoa msaada katika mwili kuliko kingine.
No comments:
Post a Comment