Winga wa kushoto wa Coastal Union ya Tanga Ibrahim Twaha ‘Messi’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuichezea Mtibwa Sugar msimu ujao
Kocha wa Mtibwa Mecky Maxime, ameiambia Goal, kwa muda mrefu alikuwa akivutiwa na kiwango cha mchezaji huyo na anafurahi kuona amefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji huyo aliyeshindwa kuisaidia timu yake.
“Nimefurahi kuwa na Twaha kwenye kikosi changu cha msimu ujao najua atakuwa na mchango mkubwa kwetu kutokana na uwezo aliokuwa nao ambao naamini pia utasaidia kuongeza ushindani wa wachezaji anaocheza nao nafasi moja,”amesema Maxime.
Maxime amesema ameamua kumsani Twaha ili kuziba nafasi ya winga wake Shizza Kichuya ambaye anatajwa kuhamia Simba msimu ujao baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba tayari ameshasaini mkataba wa awali kuitumikia timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye ligi ya msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment